SABABU ZA MWANAUME KUTOA MBEGU NYEPESI
JE, NINI KINAFANYA MWANAUME KUTOA SHAHAWA NYEPESI? Mwisho wa makala hii, tayari utakuwa umejua kwanini unapata shahawa nyepesi, kiwango cha mbegu kinachotakiwa kumpa mwanamke mimba, nini cha kufanya ili shahawa zako ziwe nzito na mbegu ziwe nyingi zaidi. JE, NINI MAANA YA SHAHAWA? Shahawa ni majimaji yanayozalishwa wakati na kutolewa wakati mwanaume anapomwaga mbegu kwenye tendo la ndoa. Shahawa zinabeba mbegu na majimaji mengine kutoka kwenye tezi dume. ZIJUE SABABU KUBWA NNE KWA NINI UNATOA SHAHAWA NYEPESI. 1. UPUNGUFU WA MBEGU Sababu kubwa ya shahawa zako kuwa nyepesi ni upungufu wa mbegu(low sperm count). Kitaalamu hujulikana kama oligospermia. Kama una mbegu chache maana yake zipo kidogo kuliko kiwango cha chini kinachohitajika kumpa mwanamke mimba. Mbegu chini ya milioni 15 kwa milliliter ndizo chache sana. BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA UWE NA MBEGU CHACHE 1. Kuvimba kwa mishipa midogo ya damu kwenye korodani mpaka kupelekea kushuka uzalishaji wa mbegu 2. Maambu...