SABABU ZA MWANAUME KUTOA MBEGU NYEPESI

 JE, NINI KINAFANYA MWANAUME KUTOA SHAHAWA NYEPESI?


Mwisho wa makala hii, tayari utakuwa umejua kwanini unapata shahawa nyepesi, kiwango cha mbegu kinachotakiwa kumpa mwanamke mimba, nini cha kufanya ili shahawa zako ziwe nzito na mbegu ziwe nyingi zaidi.


JE, NINI MAANA YA SHAHAWA?

Shahawa ni majimaji yanayozalishwa wakati na kutolewa wakati mwanaume anapomwaga mbegu kwenye tendo la ndoa. Shahawa zinabeba mbegu na majimaji mengine kutoka kwenye tezi dume.


ZIJUE SABABU KUBWA NNE KWA NINI UNATOA SHAHAWA NYEPESI.


1. UPUNGUFU WA MBEGU 

Sababu kubwa ya shahawa zako kuwa nyepesi ni upungufu wa mbegu(low sperm count). Kitaalamu hujulikana kama oligospermia. Kama una mbegu chache maana yake zipo kidogo kuliko kiwango cha chini kinachohitajika kumpa mwanamke mimba. Mbegu chini ya milioni 15 kwa milliliter ndizo chache sana.


BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA UWE NA MBEGU CHACHE 

1. Kuvimba kwa mishipa midogo ya damu kwenye korodani mpaka kupelekea kushuka uzalishaji wa mbegu

2. Maambukizi hasa magonjwa ya zinaa na kisonono

3. Vimbe kwenye korodani mpaka kuathiri uzalishaji wa mbegu

4. Homoni kuvurugika: upungufu wa homoni ya kiume ya testosterone unafanya uzalishaji wa mbegu kupungua

5. Majeraha kwenye via vya uzazi

6. Tatizo la mbegu kutotoka nje na badala yake kurudi ndani(retrograde ejaculation)

7. Matatizo ya kinga ya mwili kushambulia mbegu


JE NI Sahihi KUPATA SHAHAWA ZENYE RANGI?

Endapo utagundua shahawa zako siyo nyeupe, zina rangi ya njano ama pink basi ujue kuna shida mahali. Shahawa zenye rangi nyekundu ama pink inamanisha tezi dume yako imevimba ama pia mirisha ya kusafirisha mbegu inavuja damu.


Shahawa za njano zinaweza kuashiria uwepo wa mkojo. Na shahawa za njano na kijani zinaashiria kwamba kuna maambukizi kwenye tezi dume.


LINI UNATAKIWA KUMWONA DAKTARI?

Kama umefatilia na kuona mbegu zako ni nyepesi kwa muda mrefu, onana na daktari bingwa wa magonjwa ya wa uzazi kwa wanaume mapema

  

JE MATIBABU YA SHAHAWA NYEPESI YANAKUWAJE?

Uwezekano wa kumpa mwanamke mimba unapungua sana ukilinganisha na yule mwenye shahawa nzito. Matibabu ya changamoto yako yatazingatia na chanzo cha tatizo. 


JE NINI CHA KUFANYA  ILI KUIMARISHA SHAHAWA ZAKO?

A=Acha kuvuta sigara

B=Acha matumizi ya pombe

C- Rekebisha uzito mkubwa na kitambi kama unalo tatizo hilo

D= Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari

E=Jitahidi kudhibiti msngo wa mawazo

F= Weka ratiba ya kufanya mazoezi walau mara 4 kwa wiki


KWA WENYE TATIZO HILI WASILIANA NASI KWA +255696715467 DR LUCAS

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO

UJUE UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

TOFAUTI KATI YA PID,UTI PAMOJA NA FANGASI